Nadharia juu ya lugha ya kiswahili
Kuna nadharia mbali mbali zinazoelezea asili ya lugha ya kiswahili, baadhi ya nadharia hizo ni pamoja na
kiswahili ni kikongo
kiswahili ni kiarabu
kiswahili ni lugha ya vizalia
kiswahili ni pijini au krioli
Leo tutaangazia nadharia inayodai kuwa kiswahili ni kikongo, tutaweza pia kuangalia mapungufu au udhaifu wa nadharia hii
Kiswahili ni kikongo
Baadhi ya wataalam hudai kuwa luvha ya kiswahili asili yake ni kongo, nadharia hii hudai kuwa hapo mwanzo (zamani) pwani ya afrika mashariki haikuwa ikikaliwa na watu ma baadae kutokana na ugumu wa maisha watu kutoka misitu ya kongo ambao kwa asili shughuli yao ilikuwa ni ufugaji walifika pwani ya Afrika mashariki kupitia ujiji kutafta marisho ya mifugo yao
Madai haya hudai kuwa watu hawa kutokana na shughuli za kiuchumi walifika pwani ya Afrika mashariki wakiwa na lugha yao ambayo ni kisawhili
Madhaifu ya nadharia hii ni kwamba inashindwa kubainisha kuwa ni lini hasa hawa watu kutoka kongo walianza kuishi katikavpwani ya Afrika mashariki
bonyeza hapa kusoma zaidi