Nomino (N)
Nomino ni maneno yanayotaja vitu, watu, na hali kadhalika. Kuna aina mbali mbali za maneno ambazo ni pamoja na hizi zifuatazo:
Nomino za pekee:Nomino za pekee hutaja na kutambulisha nomino mahsusi na za kipekee. Yaani kuwa kitu ni hicho na wala si kingine chochote. Hizi ni nomino zinazohusisha majina kama vile ya watu, nchi, miji, mito, milima, maziwa na bahari. Herufi za kwanza za nomino za pekee huwa kubwa hata kama nomino hizi zinapatikana katikati ya sentensi.
Nomino za kawaida:Hizi kwa jina jingine huitwa nomino za jumla. Nomino hizi hazibainishi wazi wazi vitu ambavyo habari zake zinatolewa. Kwa mfano ikiwa ni mtu, mahsusi hatambuliwi. Haituambii kama ni Bahati, Bite ama Neema. Ikiwa ni mlima hautambuliwi kama ni Meru , Kilimanjaro au Evarest, yaani hutaja vitu bila kutaja umahususi wake kama ilivyo katika nomino za pekee.Hizi zinapoandikwa si lazima zianze na kwa herufi kubwa ispokuwa zimetumiwa mwanzoni mwa sentensi au zimetumika kama anuani ya kutajia kitu kama vile Mkuu wa Sheria. Katika mfano huu ‘sheria’ kwa kawaida ni nomino ya kawaida, lakini hapa inaanza kwa herufi kubwa kwani inataja anuwani ya kipekee.
Nomino za mguso:Nomino za mguso hurejelea vitu vinavyoweza kuhusika na mwanadamu kupitia milango ya hisia kama macho, mapua, masikio vidole na ulimi- yaani vitu vinavyoweza kushikika, kuonekana, kunusika na kuonjeka.
Nomino za jamii:Hizi ni nomino ambazo zinawakilisha vitu vingi katika jina moja, yaani nimino zinazotaja umla ya vitu vingi. Mfano; jozi ya viatu, umati wa watu, bustani ya maua, bunga ya wanyama
Nomiono dhahania:Kundi hili la nomino hutumia kigezo cha uwezekano wa kuhesabika kuziainisha. Hapa tunatofautisha kati ya nomino zinazowakilisha vitu vinavyohesabika kwa upande mmoja, na vile visivyohesabika kwa upande mwengine. Nomino ya vitu vinavyohesabikavitanda, nyumba,vikombe vitabu na kadhalika.Zile zisizohesabika hurejelea vitu ambavyo hutokea kwa wingi na haviwezi kugawika, kwa mfano maji, mate, makamasi, maziwa, moshi, mafuta. Aghalabu nomino hizo huwa sawa katika umoja na wingi.
Nomino za kitenzi jina:Hizi ni nomino zinazohusu vitenzi. Huundwa kwa kuongezwa kiambishi {ku-} cha unominishaji kwenye mzizi wa kitenzi cha kitendo halisi ili kukifanya kiwe nomino.
Vivumishi (V)
Vivimishi ni maneno yanayoelezea zaidi juu ya nomino, aghalabu vivumishi hutanguliwa na nomino. Kuna aina kadhaa za vivumushi, miongoni mwa hivyo ni pamoja na hivi vifuatavyo.
Vivumishi: vinaweza kujitokeza katika aina tatu ndogondogo.
Vivumishi vya sifa:hutoa sifa za nomino /kiwakilishi cha nomino. Sifa hizi huweza kuwa nzuri, mbaya au yoyote ile.
Vivumishi vya idadi;vivumishi vya aina hii hutoa taarifa kuhusu idadi ya nomino. Kuna vivumishi vya idadi vinavyoweza kuvumisha nomino kwa kutaja idadi ya nomino hizo kiujumla jumla bila kudhihirisha idadi halisi.
Vivumishi vya idadiambavyo huonyesha nafasi iliyochukuliwa na nomino fulani katika orodha.
Vivumishi vya kumiliki:-Ni vivumishi vinavyoonesha kuwa kitu fulani kina milikiwa na mtu au kitu kingine.
Vivumishi Vioneshi:vivumishi vya aina hii huonyesha mahali au upande kitu kilipo. Vivumishi vya aina hii hujengwa na mzizi{h}kwa vitu vilivyopo karibu na mzizi{le}kwa vitu vilivyo mbali.
Vivumishi vya kuuliza:Hivi ni vivumishi ambavyo hufafanua nomino kwa kuuliza habari zake. Hujibu swali “gani?ipi? ngapi?”
Vivumishi vya A- unganifu:Vivumishi vya aina hii huundwa kwa mzizi wa kihusishi a- unganifu. Kihusishi hiki huandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho huvumisha nomino iliyotajwa awali.Vivumishivya aina hii hutumika kuleta dhana za–Umilikaji, -Nafasi katika orodha.
Vivumishi vya jina kwa jina:Hizi ni nomino zinazotumika kama vivumishi ambazo hutumika kufafanua nomino
Vivumishi vya pekee:Vivumishi hivi huitwa vya pekee kwa sababu kila kimojawapo huwa na maana maalumu. Pia kila kimojawapo huchukua upatanisho wake wa kisarufi kulingana na ngeli ya nomino ambayo kinaivumisha.
Mizizi vivumishi hivi niote, o-ote, -enye, -enyewe, -ingine, -ingineo.
-ote:Huonyesha ujumla wa kitu au vitu-o-ote:Kivumishi cha aina hii kina maana ya “kila”, “bila kubagua”– enye:Kivumishi cha aina hii hutumika kuleta dhanna ya umilikishaji nomino fulani.–enyewe:Kivumishi cha aina hii hutumika kuisisitiza nomino fulani.– ingine:Kivumishi cha aina hii huonyesha/huonesha ‘tofauti na’ au ‘zaidi ya’ kitu fulani– ingineo:Kivumishi cha aina hii hutumika kuonesha/kuonyesha ziadi.
Vielezi(E)
Vielezi ni maneno yanayofafanua vitenzi, vivumishi au vielezi vingine. Huweza kuarifu kitendo kilichotendeka kilitendeka wapi, namna gani na hata mara ngapi.
Idadi Kamili:Vielezi vya Idadi Kamili hutaja idadi kamili ya mara ngapi kitendo kilifanyika. Kwa mfano:mara mbili, siku mbili kwa juma, mara kumi
Example 3
Gibi alimzaba kofi mara tatu na kisha akakimbiaDaktari alimwagiza mama huyo achukue dawa mara tatu kwa siku na arudi hospitalini siku mbili kwa mwezi
Idadi Isiyodhihirika:Vielezi vya Idadi Isiyodhirika huelezea kiasi ambacho kitendo kilifanyika bila kutaja kiasi kamili kwa mfano:chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani.
Example 4
Mwizi wa kuku alipigwa mara kadhaa kabla ya kuokolewa na polisi.Yeye hunipigia simu mara kwa mara.
Vielezi vya namna au jinsi
Vielezivya namna hii huonyesha jinsi au namna kitendo kilivyotendeka. Vielezi vya namna vipo vya aina kadhaa.
Vielezi vya namna halisi
Hivi ni vielezi vinavyotumia maneno ambayo kimsingi yana sura ya vielezi moja kwa moja katika uainishaji wa aina za maneno.
Vielezi vya namna mfanano
Hivi ni vieleziambavyo hutumika kufananisha vitendo na vivumishi au nomino mbalimbali. Hujengwa kwa kuongeza kiambishi(ki-)au kiambishi(vi-).Viambishi hivi hujulikana kwa jina la viambishi vya mfanano. Mfano; Ulifanyavizurikumsaidia mwanangu.
Vielezi vya namna vikariri
Hivi ni vielezi ambavyo hufafanua vitenzi kwa kurudiarudia neno moja mara mbili.
Vielezi vya namna hali
Hivi nivieleziambavyo hufafanua juu ya kitendo kilichotendeka kimetendeka katika hali gani.
Vielezi vya namna ala/kitumizi
Hivi ni vielezivinavyotaja vitu ambavyo hutumika kutendea kitendo
Vielezi vya namna viigizi
Hivi vinaelezea zaidi jinsi tendo lilivyofanyika kwa kuigiza au kufuatisha sauti inayojitokeza wakati tendo linapofanyika au kutokea.
Vielezi vya wakati
Vielezivya namna hii huonyesha wakati wa kutendeka kwa kitendo.Huweza kutokea kama maneno kamili au hodokezwa kwa kiambishi{po.}
Vitenzi
Kitenzi ni neno linaloeleza jambo lililotendwa au lililotendeka. Kitenzi huarifu lililofanyika au lililofanywa na kiumbe hai chochote kinachoweza kutenda jambo
Kitenzi cha Kiswahili huundwa na mzizi pamoja na viambishi vyenye uamilifu wa aina tofauti
Aina za vitenzi
Vitenzi vikuu:
Vitenzi vikuu ni vile ambavyo hubeba ujumbe muhimu wa kiarifu cha sentensi.
Vitenzi visaidizi:Hivi hutoa taarifa ya kusaidia vitenzi vikuu. Hutoa taarifa kama vile uwezekano , wakati, hali n.k.Vitenzi visaidizi daima hutumika na vitenzi vikuu, ndivyo vinavyobeba viambishi vya wakati.
Vitenzi vishirikishi:
Hivi ni vitenzi vishirikishi ambavyo havichukui viambishi vya nafsi, njeo ama hali. Vitenzi vishirikishi vipungufu ni vya aina mbili, ambavyo ni kitenzi kishirikishi“ni” cha uyakinishina kitenzi shirikishi “si” si cha ukanushi.
Vitenzi vishirikishi vikamilifu:
Hivi huchukuwa viambishi viwakilishi vya nafsi, njeo na hata hali. Kwa mfano;ndiye, ndio, ndipo.
Kazi za kitenzi kikuu
Kueleza tendo linalofanywa na mtenda/mtendwa.Kuonyesha wakati tendo linapotendekaKuonyesha hali ya tendoKuonyesha nafsiKuonyesha kauli mbali mbali za tendoKuonyesha urejeshi wa mtenda/mtendwa/ mtendewa/ kujitendea
Kazi za kitenzi kishirikishi
Kushirikisha vipashio vingine katika sentensiKuonyesha tabia fulani iliyopo au isiyokuwepo ya mtu fulani au kitu fullani.Kuonyesha cheo au kazi anayofanya mtu.Kuonyesha sifa za mtu.Kuonyesha umoja wa vitu au watuKuonyesha mahaliKuonyesha msisitizoKuonyesha umilikishi wa kitu chochote.
Aina za wakati katika kitenzi
Wakati uliopitaWakati uliopoWakati ujao
Hali mbalimbali za kitenzi
Hali ya mashartiHali ya kuendelea kwa tendoHali ya kutarajia, kuamuru na kuhimiza
Viwakilishi
Viwakilishi ni aina ya neno linaloweza kutumika badala ya jina/nomino .
Aina za viwakilishi
Viwakilishi vioneshi au viwakilishi vya kuonesha:
Viwakilishi vionyeshi hutumika badala ya nomino kwa kutumia kuonyesha nomino inayorejelewa bila kuitaja. Kwa mfano; huyu, yule, hapo, kule, humo. Huyu si mwenzetu kabisa; kule hakufai kwenda watoto.
Viwakilishi vya nafsi:
Kwa mfano:mimi, wewe, yeye, sisi, nyinyi, wao
Viwakilishi vya kuuliza/viwakilishi viulizi
ambavyo huashiriwa na mofu /kiambishi{-pi}ambavyo katika tungo hutanguliwa na kiambishi ngeli cha jina husika. Kwa mfano, Wangapi wameondoka? Kipi kimekosewa?
Wiwakilishi vya urejeshi
ambavyo vinajengwa na shinaambapamoja na vipande vidogo vidogo –ye-, –o-, -cho-, vyo, lo, po, mo, kon.k ambavyo vinachaguliwa kulingana na ngeli ya majina yanayorejeshwa navyo. Mfano; aliyeondoko hatapewa chake.
Viwakilishi vya idadi:
Viwakilishi hivi hutuarifu kuhusu idadi ya nomino hiyo huweza kuwa kamili (halisi) au ya jumla.Viwakilishi vya pekee/vimilikishi:-
Hivi ni aina ya vivumishi vya pekee kuwakilisha nomino. Hufuata sheria za upatanisho za nomino zinazowakilishwa. Mfano; ‘-angu, -ako, -ake, -etu, -enu, -ao ‘. kwangu haingii megini, chako haikna thamani.
Viwakilishi vya A-unganifu:- Viwakilishi hivi huundwa kwa kihusishi chaA-unganifukusimamia nomino iliyomilkiwa, inayochukuwa nafasi fulani katika orodha au nomino ya aina fulani. Kihusishi a-unganifu huandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho husimama mahali pa nomino. Mfano;ya kwakeyamemshinda,vya wazeehaviguswi.
Viwakilishi vya sifa:
Haya ni maneno ya sifa ambayo huchukua nafasi ya nomino katika setensi. Kwa mfano -eupe, -janja, -tamu
Viwakilishi vya Idadi;Idadi Kamili– hutumia namba kuelezea idadi ya nomino. ‘saba, mmoja, ishirini’ -Hutumika kusimama badala ya nomino kwa kurejelea idadi yake.
Idadi Isiyodhihirika–
huelezea kiasi cha nomino kwa ujumla, bila kutaja idadi kamili: ‘chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani’
Viunganishi
Ni maneno, kikundi cha maneno au kiambishi chenye kuunganisha maneno, kirai, kishazi ausentensi.Dhima ya kiunganishi ni kuunga vipashio viwili au zaidi vyenye hadhi sawa kisarufi.
Aina za viunganishi
Viunganishi huru:hivi ni viunganishi vinavyosimama pekee katika tungo, katikati ya vipashio vinavyoungwa.Viunganishi huru hujumuisha:
Viunganishi nyongeza/vya kuongeza,
kama vile, na, pia, pamoja. Baba na mwanae wanacheza mpira, Alichukua chakula chote pamoja na akiba iliyokuwepo.
Viunganishi vya sababu/visababishi, mfano, kwa sababu, kwa kuwa, kwa vile, madhali, ili. Alimsogelea karibu ila ambusu, Atatumikia kifungo madhali amebainika kuwa na hatia.
Viunganishi vya uteuzi/chaguo. Mfano; au, Naweza kwenda nyumani au shuleni.
Viunganishi vya kutofautisha/vya kinyume:
ila, lakini, kinyume na, japokuwa, ingawa, ilihali. Mfano; Mkumbatie lakini usimbusu.
Viunganishi vya wakati.
Wakati mfano; Mwalimu aliuliza swali wakati yeye amesinzia.
Viunganishi vya masharti;ikiwa, iwapo, hadi. Mfano; utaruhusiwa kuingia hapa ikiwa umevaa mavazi yanaostahili.
Viunganishi vihusishi;
miongoni mwa, kati ya; mfano: Jane alikuwa miongoni mwa washindi kumbi bora kitaifa.
Viunganishi tegemezi:
ni viambishi ambavyo hutiwa katika kitenzi cha kishazi tegemezi ili kukiunga na kitenzi kikuu cha kishazi huru ambavyo kwa pamoja huunda sentensi changamano au shurtia. Mfano; -po-, -cho-, -o- Nili-po-amka…, Ali-cho-mwelez…, alizo-o-neshwa…n.k
Vihusishi
Ni maneno ambayo huonyesha uhusiano uliopo baina ya neno moja na jingine. Vihusishi aghlabu huonyesha uhusiano kati ya nomino au kirai nomino na maneno mengine.
Mambo yanayoweza kuonyeshwa na vihusishi
Huonyesha uhusiano wa kiwakati; Mfano, ni vizuri kupiga mswakibaada yachakula.huonyesha uhusiano wa mahali: mfano, Ninaishikaribu nakwa Mtogolehuonyesha uhusiano wa kulinganisha: Amekulazaidi yauwezo wake.huonyesha uhusiano wa umilikaji: Usiguse hicho kitabu nicha kwanguhuonyesha uhusiano wa sababu/kiini: nimerudi kwaajili yakuonana na mkuu wa shule.
Aina za vihusishi
vihusishi vya wakativihusishi vya mahalivihusishi vya vya kulinganishavihusishi vya sababuvihusishi vya ala/kifaa mfano; -kwavihusishi vimilikishivihusishi vya namna; Kichwacha mviringovihusishi ‘na’ cha mtenda mfano, amepigwana Juma.
Matumizi ya kihusishi “kwa”
huonyesha mahali au upande: Mfano, amekwenda kwa mjomba wake.huonyesha sababu au kisababishi cha jambo: mfano; ninaishi kwa ajili yako.huonyesha wakati: mfano; sina nafasi kwa sasa.huonyesha sehemu fulani ya kitu kikubwa, mfano: Mpira umekwisha wakiwa wamefungana nne kwa tatu.huonyesha jinsi kitendo kilivyotendeka: Mfano; alimvuta kwa nguvu sana ndo maana limevunjika.
Vihisishi/Viingizi
Ni maneno ambayo hutumiwa kuwakilisha hisia fulani.
Vihusishi vinaweza kugawanywa katika makundi yafuatayo:
Vihisishi vinavyoonyesha mhemko au hisi kali
vihisishi vya furahavihisishi vya huzunivihisishi vya mshitukovihisishi vya mshangao
Vihisishi vya maamrisho au msisitizo wa jambo au tukio
vihisishi vya maadilivihisishi vya mwiitikovihisishi vya ombivihisishi vya bezovihisishi vya kutakia herivihisishi vya kukiri afya/jambovihisishi vya kiapovihisishi vya salamu