Monday, March 18, 2019

VIVUMISHI

Vivumishi  ni maneno ambayo hutumiwa kutuelezea zaidi kuhusu nomino. Aghalabu,huja baada ya nomino.

Kuna aina kadhaa za vivumishi tutakazozungumzia:

       i.            Vivumishi vimilikishi

     ii.            Vivumishi vya sifa

  iii.            Vivumishi vya idadi

  iv.            Vivumishi visisitizi

     v.            Vivumishi viulizi

  vi.            Vivumishi  vya ki-mfano

vii.            Vivumishi vya a-unganifu

viii.            Vuvumishi vionyeshi

 

VIVUMISHI VIMILIKISHI

•      Vivumishi vimilikishi hutumika kuonyesha umiliki wa nomino kwa nyingine.

Mizizi yake huundwa kwa kutumia : -angu , -etu ,-ake , -ao na kadhalika ili kuonyesha umiliki. Mf. :Gari yangu ni nyekundu

 

 

 

VIVUMISHI VYA SIFA

Vivumishi hivi hutumika kutoa sifa ya nomino mbalimbali. Mf. : kali, chungu, safi, kubwa.

Tazama sentensi hii: Yule kijana mrefuana pua kubwa.

 

VIVUMISHI VYA IDADI

•      Hutumiwa kueleza kuhusu idadi ya nomino.

•      Yaweza kuwa ya aina mbili:
  i.            Idadi isiyodhihirika:kiasi cha nomino kinatajwa kwa ujumla.Mf:chache,wastani,nyingi.

 ii.            Idadi kamili:nambari hutumiwa kuelezea idadi ya nomino.Mf:kumi,mia,elfu.

K.m: Watu wengi waliabudu sanamu lakini watatu walikataa.

 

 

VIVUMISHI VISISITIZI

•      Hutumiwa kusisitiza nomino fulani .Mf: yuyu huyu, kiki hiki, mumu humu.

•      K.m : Mzee yuyu huyu  mwenye nywele nyeupe amemwoa binti wa miaka 24.

 

VIVUMISHI VIULIZI

•      hutumika kuuliza swali na hutumia viambishi vya ngeli. Mf: -pi?

•      K.m : Jino lipi limeng’oka?

 

VIVUMISHI VYA KI- MFANO

•      hulinganisha sifa ya nomino na hali au tabia nyingine.

•      Hutanguliwa na nomino,a-unganifu na huchukua kiungo –ki. Mf.:Kijeshi, kifalme,kitajiri,kiafrika,kikazi

•      K.m: Jakie anapenda kuvaa mavazi ya kiume

 

VIVUMISHI VYA A-UNGANIFU

•      Hutuelezea zaidi kuhusu nomino kwa kuonyesha kitu kinachomiliki nomino hiyo.Mf.: la, ya, cha, za.

•      Hkiambishi cha nafsi/ngeli huambatanishwa na kiambishi –a cha a-unganifu ,kisha nomino.

•      K.m:Nguo za Daudi zilianguka alipocheza

VIVUMISHI VIONYESHI/VIASHIRIA

•      Huashiria nomino kulingana na mahali.

•      K.m:Huyu ni Peace, huyo ni Brian na yule ni Zubeda

No comments:

Post a Comment

HISTORIA YA LUGHA Nadharia juu ya lugha ya kiswahili Kuna nadharia mbali mbali zinazoelezea asili ya lugha ya ...